• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Tuesday 9 May 2017

    Dawa ya fangasi mdomoni.. Tengeneza nyumbani kwako!

    Asilimia 35-50% ya watu duniani wana fangasi mdomoni. Kuna aina nyingi wa fangasi hao lakini wale wanaoitwa candida albicans ni wengi zaidi.

    Fangasi hawa huishi bila kusababisha madhara yoyote pale ambapo mazingira ya mdomoni hayatabadilika.

    Hata watoto wadogo wanapozaliwa huwapata fangasi hawa kutoka kwenye uke wa mama zao, ndio maana mama anashauriwa kumnyonyesha mtoto Mara tu baada ya kujifungua ili ampatie kinga dhidi ya magonjwa ikiwemo hawa fangasi.

    Fangasi hawa huwa wengi sana kiasi cha kuleta madhara kwa watu wanaokula vyakula vya sukari kwa sana, wanaotumia madawa sana kama tetracycline na corticosteroids ambazo hushusha kinga ya mwili. Pia kwa wavutaji na waathirika wa UKIMWI, kisukari, saratani na wale wanaovaa meno bandia.

    Mara nyingi ugonjwa wa fangasi mdomoni (oral candidiasis/ oral thrush) inatokana na kubadilika kwa mazingira mdomoni kuliko kusema inasababishwa na wadudu.

    DALILI ZAKE
    * Vidonda au tishu za mdomoni kuharibika bila maumivu au wakati mwingine maumivu kama kuwaka moto

    * Radha ya chuma, tindikali, chumvi au uchungu mdomoni

    * Ugumu katika kumeza
    * kukwaruza kwa sauti.

    Si dalili zote zitaonekanakwa watu wote. Moja au zaidi zinaweza kujitokeza kwako.

    MATIBABU
    1. Maziwa mgando
    Maziwa mgando ni yakitumiwa na mtu mwenye fangasi mdomoni kama kinywaji kila siku asubuhi na jioni, kuanzia wiki moja na kuendelea inaweza kusaidia kurudisha hali ya kawaida ya mdomoni na kupona kabisa. Hii unaweza kufanya nyumbani kwako.

    2. Usafi wa kinywa.
    Kinywa kisafishwa kila baada ya mlo na sio kila unapoamka kama ilivyo mazoea ya watu wengi. Pia dawa inayotumiwa ni vema ikawa ni ile yenye kemikali ya kuua vimelea vya magonjwa.
    Pia kama unatumia meno sanifu hakikisha unayafanyia usafi vema kama ulivyoelekezwa.

    3. Antibiotics
    Kama kwa kutumia matibabu hapo juu hayajasaidia unaweza kutumia dawa zifuatazo kwa maelekezo ya daktari, nystalin, miconazole, gentian violet au amphotericin B.

    Share kwa wengine ujumbe huu.

    ©All rights reserved
    Dr Nature 2017

    7 comments:

    1. Mimi nata dawa ya kutibu mdomo mwekundu

      ReplyDelete
      Replies
      1. Tumia vidonge vya vitamin b mi nilikuwa na shida hiyo vilinisaidia

        Delete
    2. Jamani naombeni msaada nasumbuliwa na fangasi ya ulimi nmetumia antibiotics lakin sioni matumaini nifanyeje

      ReplyDelete
    3. Ndugu zangu nisaidieni ninasumbuliwa Sana na Hawa fangasi wa ulimi na Koo nimetumia pia antibiotics sijafanikiwa hipi Tiba sahahi

      ReplyDelete
    4. Hi naombeni msaada mtoto wangu asumbuliwa na fangasi was ulimi na Koo nimetumia dawa za antibiotic Sana ila inapunguza tu na kumrudia nifanyeje

      ReplyDelete
    5. Jamani mdomo wangu unakauka na kubabuka bila sabab yoyote nifany nn??

      ReplyDelete
    6. Mdom wangu unalua mwekundu naomben mnisaidie

      ReplyDelete