• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Friday 30 August 2019

    FAIDA ZA VITUNGUU SAUMU KWA MWANAUME NA JINSI YA KUTUMIA

    FAIDA ZA KITUNGUU SAUMU KWA MWANAUME NA JINSI YA KUTUMIA

    Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

    Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.
    Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu ( vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilisha polysulphides zilizo ndani yake kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu.
    Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali iitwayo homocystine
    mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. Kitunguu saumu kina allicin , kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzinguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi.
    Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.

    Namna ya kutumia kitunguu swaumu:

    1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja

    2. Kigawanyishe katika punje punje

    3. Chukua punje 6

    4. Menya punje moja baada ya nyingine

    5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10

    6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

    Fanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4.
     Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama unmepona tatizo lako. Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, muhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1.

    Usisahau kufanya mazoezi kegel.

    14 comments:

    1. Replies
      1. #Kegel ni neno la kiingereza ambalo linamaanisha kufanya mazoezi za sehem za siri, yaani kubana na kuachia (ii inausisha sehemu za puru na Siri) unabana na kuachia kwa dakika isiyopungua Moja, inasaidia kukomaza misuli ya sehemu za siri..
        Naitwa victor_mwasenga (professional Nurse) nitafte Facebook kwa ilo Jina kwa maelezo zaid

        Delete
    2. Kutakua na tatiz lolote kam ntatumia zaidi ya punje 6

      ReplyDelete
    3. Huwa nakula zaidi ya punje zote kwenye kitunguu Shida ni kichwa kinauma Sana

      ReplyDelete
      Replies
      1. hata mm kichwa kinauma sana hamn dawa ya kutuliza maumivu ya kichwa

        Delete
    4. Mungu akutie nguvu katika kaz yako

      ReplyDelete
    5. Asant mwandishi

      ReplyDelete
    6. Mwandishi wakti unameza unatakiwa kumeza punje ngap ndio ukalale

      ReplyDelete
    7. umesema kuwa punje 6 tukate vipande vidogo kisha nimeze baada ya hapo maji lt,1 sio mkuu

      ReplyDelete
    8. somo zuri sana

      ReplyDelete