• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Monday, 1 May 2017

    Tiba rahisi ya kisukari

    KISUKARI

    Katika miili yetu kuna mfumo tata wa mishipa ya damu tunayoweza kuichukulia kama mabomba yenye ukubwa kuanzia inchi moja (sentimita 2.5) hadi madogo kabisa ya nchi 0.0002, kiasi cha kutosha kupitisha chembe moja tu nyeupe kwa wakati mmoja.

    Damu husafirisha virutubisho vyote vinavyohitajika na kila seli katika mwili wako ili ifanye kazi sawasawa. Chanzo cha nishati kwa ajili ya seli ni sukari sahili inayoitwa glucose. Glucose (sukari) nyingi kupita kiasi inaweza kuziharibu seli. Kwa hiyo mwili una njia ya ajabu na kurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Hufanya hivyo kwa kutumia insulin, kitu kitolewacho na seli zilizo katika kongosho.


    Kisukari ni ugonjwa sugu ambapo kiasi cha sukari kinachosafirishwa na damu hakirekebishwi kama ipasavyo. Ama mwili hauzalishi insulin kawaida (kisukari namba 1 kinachojulikana pia kama T1DM), au umejenga usugu dhidi ya insulin, jambo ambalo linamaanisha sukari haidhibitiwi kwa ufanisi (kisukari namba 2, au T2DM).

    Aina ya tatu ya kisukari inaweza kutokea kwa wanawake wajawazito ambao waliwahi kuwa na kisukari kabla. Mara nyingi hutokea baada ya miezi mitatu ya ujauzito.

     Unene uliokithiri wakati wa mimba ni chanzo kikubwa cha unene uliokithiri kwa watoto. Pia huongeza uwezekano wa shinikizo kubwa la damu wakati wa mimba, na matatizo mengine ya ujauzito. Watoto wanaozaliwa na akina mama wanene kupita kiasi wana hatari zaidi ya kuwa na dosari za kuzaliwa na matatizo ya moyo.18


    Kisukari wakati wa mimba kinaweza kusababisha matatizo makubwa kwa mama na mtoto. Kiwango kikubwa cha sukari wakati wa uzazi huathiri utendaji kazi wa seli za mtoto, jambo linalosababisha kufa kwa seli na kuongezeka kwa kasoro kwa mtoto.


    Watu wenye kisukari mara nyingi hulalamika kuwa wanakojoa sana. Kiwango kikubwa cha sukari katika damu huongeza mkojo. Ongezeko la upungufu wa majimaji (na sukari) kwa njia ya mkojo huleta kiu na kuwasababisha kunywa maji mengi kujazia.

    Uzito unaweza kupungua, na uharibifu wa kudumu wa neva na mishipa ya damu unaweza kutokea. (uharibifu wa mishipa ya damu unaweza kuleta ugonjwa wa moyo, kiharusi, na figo kushindwa kufanya kazi). Kuharibika kwa mishipa ya damu iliyoachiwa inaweza kusababisha kukatwa kwa viungo.

    TIBA YA KISUKARI

    Udhibiti makini wa sukari katika damu husaidia kuzuia athari hasi za kisukari cha unene (Diabesity) na kuboresha matokeo ya hali ya ujauzito.

    Mlo usio na kabohidrati nyingi zilizosafishwa na shahamu iliyokifu, pamoja na mazoezi kiasi, vinaweza kuboresha afya ya mama na mtoto, kwa sababu mabadiliko ya namna hiyo katika mtindo wa maisha husaidia kudhibiti uzito wakati wa mimba. Kwa wanawake wanene kupita kiasi (morbidly obese) na wanataka kubeba mimba, wanapaswa kurekebisha uzito na kuzuia au kugeuza shambulio la kisukari kwa lishe na mazoezi. Kwa kufuatilia kwa makini na kufuata mipango ya afya kwa usahihi, inawezekana kuepusha kisukari cha unene na matatizo yake.


    Watu wenye kisukari hawana budi kudhibiti kwa makini kiwango cha sukari katika damu yao na wakati mwingi kuhitaji sindano za insulin—hasa katika kisukari namba 1. Baadhi ya wagonjwa wa kisukati namba 2 huhitaji vidonge vya kushusha sukari, lakini tiba ya kudumu ni kwenda kwenye mlo wa mimea wenye matunda, mboga na jamii ya karanga kwa wingi na wenye kiasi kidogo cha kabohidrati zilizosafishwa na shahamu iliyokifu. Kubadili mtindo wa maisha kama vile mazoezi na kupunguza uzito vinaweza kuzuia au kuchelewesha shambulio na kisukari namba 2.

    Habari njema.

    Tiba ya kisukari inapatikana pia katika virutubisho ambavyo vimeandaliwa kisasa kwa ajili ya kuzuia mwili kufyonza sukari kutoka kwenye chakula mtu anachokula na pia kuongeza kufyonzwa kwa chakula cha aina zingine kama protein na vitamini ili mwili utumie kwa ajili ya afya za seli.

    Virutubisho hivi ni matunda na juisi ya mimea mbalimbali ambayo imekusanywa na kuwekwa pamoja katika formula maalumu.

    Hii inasaidia sana hasa kwa kisukari aina 2. Na unaweza kupona kabisa na kuachanana na dawa/vidonge vya kila siku chini ya uangalizi wa daktari wako.
    Na baada ya hapo kuendelea na maisha yako ya kawaida.

    Soma pia hapa kwa maelezo zaidi.. Welfare jambo blog amezungumzia kwa lugha ya kiingereza

    Mtumie na rafiki yako Ujumbe huu utakuwa umemsaidia.

    Wako katika usimamizi wa afya,

    Yusufu Mohamed Filemon
    [Dr Nature]
    +255 767 759 137
    yusuphmfilemon@gmail.com

    ©Haki zote zimehifadhiwa
          >>>Dr Nature 2017

    No comments:

    Post a Comment