• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Wednesday, 23 August 2017

    VYAKULA 9 VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME


    Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.

    Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

    Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

    Sababu za Wanaume kuishiwa nguvu za kiume:

    Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

    Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka sababu ya umri. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini.

    Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. 

    Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo.

    Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.

    Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.

    Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. 

    Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. 

    Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).

    Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.

    Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.

    Kabla dakatari hajaanza kukutibu tatizo kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:

    1. Umri wako
    2. Utendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuugua
    3. Afya yako kwa ujumla
    4. Matatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote n.k
    5. Nini sababu ya wewe kutaka kupona

    Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na imani na daktari wako. 

    Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea kwenye ufumbuzi wa tatizo lako.

    Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.

    Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.

    Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

    Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

    1. Kitunguu swaumu

    Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 1 kila baada ya siku 1.

    Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti.

    Kitunguu swaumu kinaondoa sumu, kinasafisha damu, kinatibu shinikizo la juu la damu, kinashusha lehemu (kolesto) na kuzuia damu isigande.

    Pia hakikisha kila chakula unachopika basi kitunguu swaumu lazima kiwemo kama moja ya viungo na ukiweke mwishoni mwishoni kwamba kisiive sana katika moto wakati unapika hicho chakula.

    2. Tikiti maji

    Tikiti maji linasemwa kuwa ni mkuyati wa asili pia kama lilivyo parachichi. Kwenye tikiti maji kuna vitu hivi vitatu mhimu sana kwa afya ya mapenzi navyo ni ‘lycopene’, ‘beta-carotene’ na ‘citrulline’ ambavyo husaidiwa kuweka mishipa ya damu katika hali ya utulivu.

    Tikiti maji ni dawa ya asili inayoweza kutumika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa watu wa jinsia zote mbili bila kukuacha na madhara yoyote mabaya.
    Kula tikiti maji kila siku na unapokula tafuna na mbegu zake kwa matokeo mazuri zaidi.

    3. Ugali wa dona

    Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume.

    Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.

    4. Chumvi ya mawe

    Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.

    5. Maji ya kunywa

    Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.

    6. Mbegu za maboga

    Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.
    Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

    Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili.

    Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia

    Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako.

    Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.

    Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

    Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

    Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

    Unaweza pia kutumia unga wa mbegu za maboga vijiko vikubwa viwili kutwa mara 1 ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani.

    7. Asali na Mdalasini

    Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una kalsium, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).

    Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga ya mwili. Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.

    Jaribu na uone tofauti! Changanya vijiko vikubwa vitatu vya asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu na uache mchanganyiko huo kwa dakika 15 hivi.

    Kunywa nusu glasi asubuhi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu nyingine kabla ya kwenda kulala kwa siku kadhaa hata wiki kadhaa.

    Namna ya kuandaa na kutumia Asali yenye Mdalasini?

    Kwenye lita 1 ya asali ongeza vijiko vikubwa vitano vya mdalasini ya unga na ukoroge vizuri kabla ya kuutumia. Uhifadhi mchanganyiko huu kwenye bakuli kubwa ili iwe rahisi kuukoroga tena vizuri kila unapotaka kuutumia.

    Unaweza kuutumia katika maji au wenyewe kama ulivyo ukipaka juu ya ngozi au ukitumia kwenye vyakula kama mkate na kadharika. Kama utakunywa basi vijiko vikubwa vitatu ndani ya maji ya uvuguvugu glasi moja kwa siku inatosha.

    Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala.

    Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

    8. TANGAWIZI

    Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.

    Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa.

    Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.

    Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje.

    Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!

    9. Parachichi

    Parachichi hujulikana pia kama mkuyati wa asili. Parachichi ni dawa ya asili ya kuamsha hamu ya tendo la ndoa. Hapa Tanzania maparachichi yanapatikana kwa wingi sana mkoa wa Kilimanjaro na hata Mbeya pia.

    Potasiamu husaidia kuongeza ufanisi wa kazi wa tezi ya ‘thyroid’ ambayo yenyewe husaidia kuongeza hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa kama itakuwa ipo kwenye usawa wake mzuri.

    Vitamini B6 huhamasisha uzalishwaji wa homoni za kiume na ‘folic acid’ ni mhimu katika kuwezesha umeng’enywaji na kuweka sawa usawa wa protini mwilini.

    Kula parachichi moja kila siku. Unaweza pia kunywa juisi ya parachichi kikombe kimoja kila siku ukiongeza asali vijiko vikubwa viwili ndani yake.

    Kwa matokeo mazuri na yanayodumu tumia hivi vyakula vyote kila siku.

    Karibu tena natutefreeclinic.blogspot.com

    No comments:

    Post a Comment