• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Tuesday, 22 August 2017

    HII NDIO SABABU MOJAWAPO BAADHI YA WATOTO WA KIUME WANATABIA NA MAMBO YA KIKE, NA WANAWAKE KUWA NA MAUMBILE NA TABIA ZA KIUME



    Lengo la makala haya sio kutusi watu wenye madhaifu haya Bali ni kutoa elimu ili tujikinge na hali kama hizi siku za usoni kwa sababu hata wao hawakutaka kuwa hivyo, ndio sio uchaguzi wao.

    Sehemu kubwa ya jamii yetu hutumia plastiki katika matumizi mengi sana. Hata hivyo plastiki imegawanyika katika aina kuu 2.

    1. Plastiki ngumu
    Hutumika kutengenezea ndoo, sahani, beseni, kanda mbili, viatu, chupa za maji n.k

    2. Plastiki laini
    Hutumika kutengenezea mifuko ya Rambo, mifuko ya maji ya uhai n.k

    Kwa kweli plastiki inamatumizi mengi sana, wengine hutumia kuwashia mkaa wanapohitaji kupika, na wengine hufunikia vyakula kama wali na viazi ili chakula kiive vizuri.

    Wengine huchemsha maji na kuyaweka kwenye ndoo ya plastiki, wengine hunywea chai au uji kwenye kikombe cha plastiki.. Huruma kwa wanafunzi wa bweni vifaa Vingi vya kulia chakula ni vya plastiki tena wanakula chakula kikiwa cha motomoto😌

    Ukizunguka mtaani takataka zinaozoongoza ni plastiki na maeneo mengine plastiki ni nyingi kuliko hata majani😌

    Na hivyo inafikia wakati plastiki hizi huchomwa ili kuweka mazingira safi.

    "Dr Nature nini unachojaribu kusema?"

    PLASTIKI YOYOTE INAPOPATA JOTO/KUCHOMWA HUTENGENEZA SUMU YA KUTISHA!

    Sumu hii inaitwa DAYOKSINI, Kwa kitaalamu huitwa 2,3,7,8-tetrachlorodibenzoparadioxin. 😂 Achana na hilo jina refu kama nini, waachie akina ngoswe!

    Sumu hii ni ya pili kati sumu hatari zinazozalishwa na binadamu duniani, inafuata ile itokanayo na taka zenye mionzi ya sumu ya radioaktivu.

    *INAKUWAJE SUMU HII INAINGIA MWILINI*
    Kila plastiki inapopata Joto la kutosha au inapochomwa huzalisha sumu ya DAYOKSINI.

    Sumu hii inaweza kuingia mwilini kwa kutumia pua na mdomo.

    Ile ambayo itaenda hewani hufuata njia 2.
    a) Hupeperushwa kwenye hewa mpaka mamia ya kilometa. Huko hunata kwenye majani ya mimea na mazao mbalimbali. Ng'ombe, mbuzi, nguruwe na wanyama wengine hula sumu hii ambayo huwaingia na kutuama kwenye seli zenye asili ya mafuta katika miili ya wananyama hawa.

    b) Nyingine hupeperushwa na kuishia kwenye miti, maziwa na bahari na vyanzo mbalimbali vya maji. Huko nako kuna wanyama kama samaki na wadudu wengine hupata dozi ya sumu na kukaa nayo katika seli zao zenye asili ya mafuta. Siku nyingine Dr Nature atakula samaki au mnyama huyu na kupata dozi ya kutosha ya sumu hii.

    Sumu hii inapoingia mwilini inapenda sana sana seli zenye asili ya mafuta. Sumu hii huenda na kukaa kwenye kiini cha seli na kujichanganya na kuwa kama sehemu ya seli ndicho kinachoongoza kuamua mtu awe wa aina gani. Yaani awe mzungu, mhindi, cheusi au afanane na baba au mama, chotara, mbilikimo, mwenye magonjwa n.k

    Sumu hii hubadili Tabia ya mwili na kuifanya iwe tabia inazotaka yenyewe ambazo zinadhara kiafya. Kwa sababu inabadili mchanganyiko wa asili wa kiini cha seli, sumu hii inaweza kuleta magonjwa ya kurithi katika familia.

    *MADHARA YANAYOTOKANA NA SUMU YA DAYOKSINI*
    Hapa sasa tega sikio vizuri..

    1. HUPUNGUZA KINGA YA MWILI DHIDI YA MAGONJWA MBALIMBALI.
    Kwa sababu seli nyeupe (maaskari wa mwili dhidi ya magonjwa) hulewa, sumu na dawa inayotengenezwa kushindana na maadui wengi pia hupungua. Ndio maana utakuta watu wengi sana wanaugua bila sababu za maana!

    2. HUSABABISHA MIMBA KUHARIBIKA NA MFUMO WA UZAZI WA KAWAIDA KUHARIBIWA.
    Sumu hii hupunguza uwezo wa uzazi na kupoteza uwezo wa kuchukua mimba kwa miezi 9, nyingi hutoka kabla ya muda huo. Mmh! Ni ngumu kupata mtoto au akizaliwa anakuwa njiti au mwenye ulemavu wa kudumu wa viungo na/au akili. Mf. Spina bifida ambapo mtoto huzaliwa bila mifupa kadhaa ya uti wa mgongo.

    3. HULETA MATATIZO YA MFUMO WA NEVA ZA FAHAMU.

    4. HUSABABISHA UGONJWA WA MFUKO WA KIZAZI (ENDOMETRIOSIS).

    5. HUSABABISHA KUJISIKIA UCHOVU TU SIKU ZOTE BILA SABABU YA MSINGI (CHRONIC FATIGUE SYNDROME)

    6. HULETA MAGONJWA MBALIMBALI YA DAMU.

    7. HUSABABISHA KANSA ZA AINA MBALIMBALI
    Sumu hii huleta kansa katika dozi ndogo sana inayoweza kudhaniwa haiwezi kuleta madhara. Sumu hii huwa inauwezo wa kuhamasisha uzalishaji wa seli kichaa za kansa kwa sababu huzibadili tabia homoni zinazohusika na ukuaji.

    Sumu hii huzifanya seli ziwe nyingi isivyo kawaida. Badala ya kugawanyika na kuzikuza kwa kawaida ili MTU aonekane na kuongezeka (yaani kukua), zenyewe huzifanya zigawanyike zikiwa seli mbovu zenye kichaa (yaani zenye tabia isiyorekebishika) zinazozaa haraka kuliko kawaida; hizi ndizo zinazoitwa kansa.

    *8. HUHARIBU HOMONI ZA MWILI*
    Hapa sasa angalia kwa makini❗

    Homoni ni kemikali nzuri za mwili ambazo hutengenezwa sehemu moja ya mwili na kusambazwa kwenye damu ili irekebishe kazi za mwili ziende vizuri. Mfano, mwanamke awe na sauti ya kike, ngozi laini ya kike, sura ya kike, n.k, ni lazima awe na homoni hizi.

    Hali kadhalika ili mwanaume awe na ndevu, sauti ya kiume, misuli ya kiume na vinginevyo vya kiume lazima ziwepo kwa ajili ya hiyo. 

    Sumu ya DAYOKSINI huharibu homoni hizi, hapo sasa unaweza ukamkuta mwanaume ana tabia ma mambo ya kike au mwanamke ana tabia na mambo ya kiume. 

    Kwa sababu sumu hii inaweza kurithishwa, watoto wa kiume wanaobahatika kuzaliwa huwa na homoni za kiume kidogo kuliko kawaida, na baadaye huwa na uwezo mdogo (kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha homoni ya testosterone) wa kuzalishwa mbegu za kiume.

    9. WATOTO WANABAHATIKA KUZALIWA WAKIWA NA SUMU HII:
    a) hawana uwezo wa kutosha katika masomo yao 

    b) makuzi ya watoto hawa yanaathirika kwa sababu tezi ya makuzi (thyroid gland iliyoko nyuma ya mbele ya shingo) huathirika kwa sumu hii.

    *KIASI GANI CHA SUMU HII KINATOSHA KUKUATHIRI?*
    Hakuna kiasi maalumu ambacho mtu lazima akifikie ndipo aweze kupata madhara kiafya, kiwango kidogo tu kinaweza kuleta madhara makubwa.

    *LAKINI MBONA INI LIPO, LINAWEZA KUIONDOA ISILETE SHIDA....!!!???*
    Mwili wa binadamu hauna kinga dhidi ya sumu hii. Jambo lingine baya ni kwamba mwili hauwezi kuiharibu sumu hii kama unavyoweza kuharibu sumu zingine kupitia ini, tena inapoingia haitoki kwa haraka kupitia njia za kawaida za kuondoa sumu kama figo. 

    Husababisha ugonjwa wa ini lenyewe. Inaeleweka kwamba mtu hawezi kuishi bila ini, tena magonjwa mengi ya ini ni vigumu kuyatibu.

    Angalia hapa, huharibu insinereta, yaani nyumba maalumu inayotumika kuchomea taka. Inatishia afya na maisha ya binadamu lakini haijapewa kipaumbele.

    *DR NATURE UNAUHAKIKA GANI NA HAYA MAMBO?*🤔🤔

    Utafiti uliofanywa kwa wanyama wa porini waliopewa sumu hii kwa kiwango kidogo sana unaonesha kuwa walipata kansa za viungo mbalimbali zikiwemo kansa za INI, tezi za adrenali, thairoidi, ngozi, mapafu, pua na kinywa. 

    Kinga dhidi ya magonjwa iliharibika kwa maisha yao yote, pale ilipojaribiwa kwa wanyama wenye mimba kwa kutoa sumu hii dozi moja kwa kiasi kidogo, mimba ziliharibika.

    *SASA TUFANYEJE MAANA.,..!! DUUHH!!*🤷‍♂
    Usipate shida wala kuhangaika, ndio maana nimekuletea somo hili vinginevyo ungezidi kuangamia pole pole.

    Haya niapendekezo yangu kama Dr Nature ili tuwe sehemu ya suluhisho ya tatizo hili.

    1. JITIHADA ZA MAKUSUDI ZINAHITAJIKA KUTUMIKA
    Kuwaletea somo hili ni moja kati ya jitihada zangu za makusudi kuwaelimisha kuhusu tatizo hili

    Kuondoa tatizo hili katika jamii masikini, inahitaji nguvu ya kutosha na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, kuanzia mtu binafsi, jamii, syangu. kama afya, mazingira na wanasiasa.

    Lakini wewe binafsi unasehemu kubwa ya kufanya, EPUKA KUVUTA MVUKE/MOSHI UNAOTOKANA NA PLASTIKI YENYE VITU VYA MOTO AU INAYOUNGUA!

    Kwa sababu ile inayopatikana kwa njia isiyo ya moja kwa moja kama kula wanyama au mimea iliyoathirika na sumu hii haina nguvu sana kama ilivyo hii unayoipata moja kwa moja kwa kuivuta.

    Epuka sana kadri iwezekanavyo kula mafuta ya wanyama  au nyama yenye mafuta mengi😌 yatakuua rafiki yangu.

    2. KUONDOA SUMU KWA NJIA YA ASILI.
    Njia nilifundisha hapa siku chache zilizopita, unaweza ukaisoma hapa>>>>>>>>

    https://naturefreeclinic.blogspot.com/2017/08/kufunga-na-afya.html

    3. NJIA MARIDADI YA KUONDOA SUMU
    Hapa sasa ni kujaribu kunusuru kwa haraka sumu nyingi mwilini. Kabla hujauburudisha mwili wako kwa hii wasiliana nami ili kupata maelekezo namna ya kuipata.

    Aidha husaidia kuongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa, huimarisha mfumo wa chakula.. Ooh mwili wako ungeweza kuongeza ungekwambia "NAHITAJI PIA"😊

    *Nature Treats Love Heals*

    ©Dr Nature
    real.dr.nature@gmal.com
    +255767759137

    No comments:

    Post a Comment