• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Tuesday, 25 April 2017

    KINGA NA TIBA YA TEZI DUME


    KILA MWANAUME MWENYE UMRI WA MIAKA 40+ YUPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA TEZI DUME.

    PROSTATE GLAND (TEZI DUME).
    Ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume.Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra). Ina umbo la yai,ina ukubwa wa kawaida japo ukubwa huongezeka kadri umri unavyoongezeka.

    Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la kujamiiana(sex).
    Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.

    SEHEMU KUU ZA TEZI DUME.

    1.PERIPHERAL ZONE(SEHEMU YA NJE)
    ~Hii ni sehemu ya nje ya tezi ambayo madakari wengi hutumia hii tezi kubaina kama kuna tatizo kwenye tezi kwani ni virahisi kiugusa kama daktari akiingiza index fingure(kidole cha kusontea) kwenye njia ya haja kubwa. Kukua kwa sehemu hii hakuwezi kuathiri utokaji wa mkojo.

    2. TRANSITIONAL ZONE(SEHEMU YA KATI)
    ~ Hii ni sehemu ya tezi ambayo ikikua yani ikiongezeka ukubwa tunasema KUVIMBA KWA TEZI TUME kitalamu BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH) kuna uwezekano mkubwa wa tezi dume iliyovimba kuzuia njia ya mkojo kupita. Kwani ndio sehemu ya tezi iliyo karibu kabisa na njia ya mkojo. Mara nyingi hii sehemu ikikua ndio inayo sababisha matatizo ya kukojoa(obstructive symptoms).
    Tezi hii pia daktari anaweza kuibaini kwa kutumia kidole kipimo hiki huitwa DIGITAL RECTAL EXAMINATION(DRE)
    hii ni kwa sababu ikikua inasukuma ile sehemu ya pembezoni yani peripheral zone kuelekea njia ya haja kubwa. Hivyo dakatri anaweza kubaini kama tezi imekua au laa.

    KUKUA KWA TEZI DUME.
    Kukua kwa tezi ya kiume kitalamu tunaita BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH).
    Hili tatizo mara nyingi huanza baada ya miaka 40 hivi na dalili huja kujionesha uzeeni. Na mpaka mtu apate Cancer ya Tezi Dume,basi huyo mtu amekua na tatizo la tezi dume kwa zaidi ya miaka 10.
    Hivyo tezi inaweza ikawa kubwa sana lakini haina dalili, hii ni kutokana na sehemu gani ya tezi iliyovimba au kuongezeka.
    Tezi inapoonesha dalili jua tatizo hilo ni sugu na liko katika hali mbaya.

    DALILI ZA KUVIMBA KWA TEZI DUME.
    1. Kukojoa mara kwa mara
    2. Kubakiza mkojo kwenye kibofu.
    3. Kukujoa sana usiku
    4. Maumivu wakati wa kukojoa na mkoja usioenda mbali.
    5.Kupungukiwa nguvu za kiume
    6. UTI ya mara kwa mara
    7. Mawe kwenye kibofu kutokana na mrundikano wa mkojo.
    8. Figo kujaa maji. Hii ni kwasababu mkojo huo unarudi nyuma kuelekea figo(hydronephrosis)
    9. Kupoteza fahamu(uremia)
    10. Mapaja kuumwa

    HIZI DALILI NIMEZITAJA KULINGANA NA TATIZO LINAVYOKUWA SUGU KWA MGONJWA HIVYO UGONJWA HUU NI HATARI USIPO WAHI.

    JINSI YA KUBAINI KUVIMBA KWA TEZI.
    ~Kumbuka BPH sio kansa ni uvimbe tu wa kawaida wa tezi lakini kumbuka tezi hii inaweza kuvimba pia kutokana na kansa ya tezi dume (prostate cancer).

    1. Uchunguzi wa kawaida kwa kutumia kidole kupitia njia ya haja kubwa kuangalia kama tezi ina tatizo. Kipimo hiki huitwa DIGITAL RECTAL EXAMINATION. Baada ya kipimo hicho daktari huandika alicho kigusa kama ni ugonjwa au iko kawaida.

    2. Hiki ni kipimo cha kupiga picha kibofu cha mkojo kinaitwa CYTOSCOPE. Kumbuka kipimo hiki una ingiziwa waya flani wenye tochi mbele kwenye njia ya mkojo huku huo waya umeunganishwa kwenye screen. Hivyo chochote huo waya utakacho murika kitaonekana kwenye screen.
    Ubaya wa hiki kipimo ni kwamba kinaweza kuumiza kuta za njia ya mkojo na baada ya wiki kama mbili njia inaweza kuziba jeraha linapo pona. Ila ni kipimo kizuri sana.

    3. Kipimo kingine kinaitwa RECTAL UTRASOUND hiki ni kipimo cha kupiga picha kupitia njia ya haja kubwa (rectal) na kutoa picha kwenye jarida gumu kumsaidia daktari kusoma.

    4. Kipimo cha kutofautisha kati ya uvimbe wa kawaida(BPH) na kansa(PROSTATE CANCER).
    Kipimo hiki kinaitwa PROSTATIC SPECIFIC ANTIGEN. Hii ni protein inayotolea kwa wingi endapo kuna kansa ya tezi dume. Hivyo damu ya mgonjwa itachukuliwa na kupelekwa maabala kuchunguza kama ni nyingi kupita kiasi kwenye damu. Kama hii protein ipo kawaida basi uvimbe huo sio kansa ni BPH. Lakini kama kiwango ni kingi uvimbe huo ni KANSA. Hivyo uchunguzi zaidi unahitajika kama kuchukua sample ya kinyama kutoka katika tezi na kupeleka maabala.

    MATIBABU YA KUKUA KWA TEZI DUME.

    1. Tezi dume kama haina dalili zozote mara nyingi huwa haishughulikiwi sana hospitali lakini dawa za kupunguza kasi anaweza pewa mgonjwa. Lakink ni mara chache.
    2. Kama tezi imesha anza kuleta dalili kama usumbufu wakati wa kukojoa siku hizi kuna operation ya bila kukata inaitwa TRANSURETHRAL RECTIONING OF PROSTATE AU CHANNEL TURP.
    Hii operation inafanywa kama akiwa anafanya kipimo cha CYSTOSCOPE. Lakini hapa anaweka wire mbele kiko cha mviringo kinapitishwa kwenye njia ya mkojo kina enda kukata kinyama kinachoziba, i mean tezi iliyovimba. Hapa inazibua njia ya mkojo ili mtu akojoe. Ukifanyiwa operation hii vizuri tezi hujirudia baada ya miaka kama 3-5 tangu siku ya operation.

    MADHARA YA TIBA HII
    1. Kukosa uwezo wa kufikia kishindo yani hutoi shahawa(RETROGRADE EJACULATION) wazee wengi hulalamika sana baada ya hii operation hivyo ushauri nasaha lazima utolewe ili mgonjwa ajue nini madhara yake kabla ya operation.

    2. Kuziba kwa njia ya mkojo kutokana na kuumia kwa njia hizo wakati wa kitendo hicho. Panapokua panapona hilo kovu linaziba njia ya mkojo.

    3. Operation kubwa ya kuondoa tezi hio hufanyika kwa kufungua kibofu cha mkojo na kutoa hiyo tezi. Madhara ni mengi sana kuhusu hii bora ile namba mbili.

    UTAFITI UNASEMA NINI KUHUSU KUKUA KWA TEZI NA NAMNA YA KUJIKINGA NAYO.

    #NOTE: CHANZO CHA KUKUA KWA TEZI DUME.
    - Utafiti unaonesha chanzo kikuu cha kukua kwa TEZI DUME ni upungufu wa virutubisho na madini muhimu sana ya ZINK,IRON na LYCOPENE. Na hii ni kwasababu mwili unashindwa kujisupport/kujisaidia wenyewe kupata hivyo virutubisho kutoka kwenye vyakula tunavyokula kadri umri unavyoongezeka.
    Hivyo lazima tupate supplement/virutubisho vya ziada.

     LYCOPENE.
    -Hivi ni virutunisho vinavyotokana na nyanya,hivyo mwanaume anasahuriwa kula(kutafuta) nyanya 8 kila siku.
    Lycopene ina uwezo wa kupenya kwenye tezi dume na kuondoa tatizo lolote na kuzuia kabisa kukua kwa tezi dume. Pia ina uwezo mkubwa wa kuzuia kansa ya tezi dume.

    Hivyo tunashauri kila mtu mwenye umri wa miaka 30 na kuendele atumie virutubisho hivi ili kujilinda na tezi kukua. Utumiapo lycopene,Madini ya Zink na Iron ambayo yametengenezwa kwa kiwango kingi(concentrated) kuna uwezekano mkubwa wa kutopata kabisa tezi hii dume hata kama kwenye ukoo wenu wote walipata tezi hii.

    #Note: Watu wazima wengi wanaogopa kusema kama wana tatizo hilo,mpaka tatizo linapofikia kwenye hatuna mbaya sana,hivyo kama una kaka,mume au baba mwenye umri wa kuanzia miaka 40+ usisubiri akuambie,mtafutie Kinga mapema.

    No comments:

    Post a Comment