• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Wednesday, 11 October 2017

    Kemikali Inayosababisha Saratani Huenda Ipo Kwenye Maji Ya Kunywa


    Watafiti wameanza kujikita katika dioxane, kemikali hatari inayoanza kuonekana kwenye maji ya bomba. Huenda hujawahi kuisikia kemikali hii dioxane lakini kuna uwezekano mkubwa umewahi kuinywa.

    Dioxane, kikemia huitwa 1,4-dioxane, ni kiyeyusho cha kiwandani kinachotumika kutengeneza bidhaa aina nyingi zikiwemo vipodozi, vanishi, rangi, na dawa za usafi.

    Wakala wa kulinda mazingira wa Marekani, hupatia daraja la kemikali inayoweza kusababisha saratani, kemikali hii ya dioxane. Kulingana na ripoti iliyotolewa Septemba 2017 na Kikundi cha Mazingira walipata kuona dioxane katika maji ya bomba ambayo huathiri watu milioni 90 katika majimbo 45. Hadi sasa hakuna utafiti wowote kuhusu kemikali hii uliofanyika hapa kwetu Tanzania.

    Hata hivyo, dioxane imefahamika kuweza kuathiri ini, figo na kuwa na uwezo wa kusabababisha saratani.

    Samahani sina lengo la kukutisha! Maji ni uhai. Tumezungukwa na mazingira yaliyochafuka sana kwa sumu, lakini bado tuna nafasi ya kufanya tukawa salama. Tii kanuni za afya kadri inavyowezekana na matatizo kama haya yasiyoepukika yatazimwa kwa namna usiyojua. Mfano; kama ukipata vyakula vyenye vitamini E, A na C kwa wingi vitakusaidia kupambana na magonjwa ya saratani. Ukifanya mazoezi kwa uaminifu na kunywa maji ya kutosha, na ukaepuka pombe magonjwa ya ini na figo utayaepuka.

    Tuambie wewe unalizungumziaje suala hili......

    Nature Clinic tunakutakia afya njema!

    No comments:

    Post a Comment