• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Wednesday, 11 October 2017

    AJABU! Dawa Ya Kutibu Dawa

    Usugu wa madawa ni hali inayotokea pale ambapo mwili unakuwa na ukinzani wa kupona ugonjwa fulani kwa kutumia dawa iliyozoeleka. Mfano, ulizoea kila ukiugua kichwa unatumia vidonge 2 vya panadol na kinatulia. Usugu unakuja pale ambapo unatumia vidonge hivyo 2 lakini bado hali haibadiliki.
    Tatizo hili limekuwa sugu sio tu Tanzania bali dunia nzima kutokana na matumizi ya madawa ya kisasa.

    Viongozi wa dunia wameagiza kutengezwa kwa dawa kwa ajili ya usugu wa madawa. Wanasema kwa sasa hakuna dawa za kutosha kupambana na tatizo hili. Katika habari iliyotolewa mwishoni mwa mwezi Septemba 2017, maafisa wa Umoja wa Mataifa (UN) na Shirika la Afya la Dunia (WHO) walisema dawa nyingi wanazotengeneza sasa hivi ni marekebisho tu ya dawa zilizopo na haziwezi kufanya kazi kwa muda mrefu.

    Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus mkurugenzi mkuu WHO katika taarifa hiyo alisema, "Usugu wa madawa ni dharura ya dunia nzima katika afya ambayo itatishia sana maendeleo ya tiba ya kisasa (modern medicine)"
    Kwa kadri muda unavyosonga, vimelea vya magonjwa katika miili ya binadamu hupata uwezo wa kupinga madawa ambayo hapo awali yaliwashinda. Vimelea wanapokuwa wapinzani kwa dawa, husambaa kwa wepesi zaidi.

    Dr Ju, profesa msaidizi idara ya maikrobiolojia The Ohio State chuo cha Wexner Medical Center anasema "Hili ni tatizo kubwa mno" "Kufikiria kuhusu ugunduzi wa dawa, bidhaa za asili ni vyanzo vipya vya dawa (pharmaceuticals) katika kizazi kijacho".
    Huchukua muda mrefu sana na hatua nyingi kutoka kugundua dawa, kufanyiwa majaribio hadi kuingia sokoni. Hii imekuwa ikiwarudisha nyuma wagunduzi wengi na makampuni mengi yanayojishughulisha na ugunduzi wa dawa.

    Dr Ju aliongeza kuwa "tumesikia kwamba zama za dhahabu za ugunduzi wa dawa, tulipokuta kuwa dawa nyingi tunazotumia leo, zilikuwa ni miaka ya 1940-1950.
    Dr Nature anasema, ni vema kuchukua tahadhari kabla ya hatari.
    • Usitumie dawa bila kupata maelekezo ya kitaalamu kutoka kwa mtaalam wa afya aliyethibitishwa.
    • Tumia dozi ya dawa utakayopewa na umalize bila kujaliisha unajisikia vizuri au vipi vinginevyo upate maelekezo kutoka kwa daktari wako.
    Mungu ametupatia katika mazingira yetu kila kitu tunachohitaji kwa ajili ya afya zetu. Lakini kuvunja sheria za Mungu na sheria za mazingira ndicho ambacho kimetuweka katika matatizo yote haya. Ndio, tukizitii sheria zake na kuheshimu asili na sheria zake shida hizi tutazisikia kwenye vyombo vya habari.

    Mambo haya yanapoendelea ni busara kutafakari kwa busara, hekima iliyopo katika unafuu na ubora wa dawa za asili na mbadala.
    Rafiki yetu wewe una maoni gani katika hili? Tafadhali tushirikishe maoni yako.

    Imeandaliwa na Nature Clinic. Tunakutakia afya njema!

    No comments:

    Post a Comment