Hali ya kufunga choo hutokea iwapo utumbo mkubwa uyashindwa kufanya kazi yake kikamilifu ambao ndio mkondo wa mwisho wa kupitishia chakula.
Chanzo cha kufunga choo
1. Kula vyakula vilivyokobolewa2. Kula vyakula vilivyokaangwa sana
3. Kutokunywa maji ya kutosha
4. Utumiaji kwa wingi wa chai na kahawa
5. Kula kuliko kiasi
6. Kula vyakula visivyofaa kiafya
7. Kutokuwa na muda maalumu wa kula (kula ovyo ovyo)
8. Utumiaji kiholela wa dawa za kuhara
10. Udhaifu wa misuli ya utumbo
11. Kutokuwa na mazoezi ya kutosha
12. Shinikizo la kihisia (depression)
Dalili za ugonjwa wa kufunga choo
1. Kutoenda choo Mara kwa Mara angalau Mara moja kwa siku2. Kutoa kinyesi ambacho ni kigumu sana
3. Harufu mbaya mdomoni
4. Kukosa hamu ya kula
5. Kuumwa kichwa na kujisikia kizunguzungu
6. Kuumwa mgongo, kiungulia, kukosa usingizi n.k
Tiba ya Shida ya kukosa choo
Ziko tiba nyingi za asili na hii ikiwa ni mojawapo, lakini jambo la kwanza zingatia kanuni za afya ili kuepuka vyanzo vya ugonjwa huu kama nilivyoviorodhesha hapo juu.👉 Kula ½ kilo ya papai kila asubuhi kwa muda wa Siku 7. Papai husaidia kulainisha choo na kuondoa hali hiyo.
👉 Chukua kilo moja ya spinachi. Saga/pondaponda na ongeza maji Lita 1 ili kutengeneza juisi ya spinachi.
Kunywa glass moja ya juisi hii asubuhi na jioni kwa muda wa Siku 10.
Sio lazima utumie vyote papai na spinach kwa dozi unaweza ukatumia mojawapo tu inafaa.
Kama ukichelewa kutibu ugonjwa tatizo hili unaweza kupata shida zingine kama kidonda kwenye njia ya haja kubwa (anal fissure) na bawasiri.
Kidonda kwenye njia ya haja kubwa na tiba yake (ANGALIA VIDEO HAPA)
#Kula chakula sahihi kwa kiwango sahihi, muda sahihi na ukiwa na hisia sahihi | Eat right type of food in right amount at right time with right state of mind
Je, unachochote unatamani tufahamu pia kuhusiana na kukosa choo? Kama ni swali, nyongeza au maoni andika comment hapa chini.
©Dr Nature | Your friend
No comments:
Post a Comment