Katika ulimwengu huu
wa mtandao matumizi ya laptop na simu yamekuwa ni muhimu sana na huwezi
kuyatenganisha na shughuli zetu za kila siku. Lakini kwa bahati mbaya watu
wengi wamekuwa wakivitumia vifaa hivi bila tahadhari ya afya ya uzazi.
Utafiti uliofanyika
na kuchapishwa na shirika la kimarekani ambao ulihusisha vijana 29 wenye umri
miaka 26-45. Kila kijana alitoa shahawa ambazo ziligawanywa katika makundi 2.
Kundi la kwanza liliwekwa mahali penye Wi-Fi ya laptop na kundi lingine lilitumika
kulinganisha.
TAZAMA VIDEO HAPA
Lengo ilikuwa ni
kupima athari ya Wi-Fi katika mwendo wa seli za uzazi (spamu), uwezo wa
kuzalisha na athari katika vinasaba (DNA) vya seli hizo.
Baada ya masaa 4 ilionekana
kwamba ¼ ya mbegu zilizokuwa zimewekwa kwenye Wi-Fi hazikuwa na uwezo wa
kuogelea (hazina uwezo wa kuzalisha).
Mionzi ya
ememe-usumaku (EMW) ya kama ya Wi-Fi na aina nyingine yoyote inaweza kuleta
athari katika uzalishaji wa seli za uzazi kwa wanaume. Mamilioni ya seli za
uzazi huzalishwa kila siku katika
korodani (kiwanda) na hivyo mionzi hii inapokuwa mingi na karibu na eneo hili
kwa muda mrefu inapelekea vinasaba vya seli hizi kuathiriwa na kusababisha
idadi ndogo sana ya seli hizi kutengeneza (low sperm count) au seli ambazo
zitatengenezwa zinaweza kuwa na ulemavu kiasi kwa namna ya maumbo na utendaji
kazi zisiweze kurutubisha.
Tabia ya kupaka
laptop mapajani wakati wa matumizi huleta joto katika korodani na hivyo
kuathiri uzalishwaji wa mbegu za uzazi. Hii ni sanjari na kuoga maji ya moto
kila siku, kuendesha vyombo vya moto kama pikipiki na magari kwa muda mrefu,
kuvaa nguo zinazobana sana na tabia zingine zenye kusababisha joto katika
korodani.
Dr Wanyoike, mtaalamu
wa afya ya uzazi anasema kumbukumbu zinaonesha kwamba tatizo la utasa kwa
wanaume unaosababishwa na kuwa na mbegu kidogo limeongezeka sana hasa katika
miaka ya hivi karibuni huenda ni kwa sababu ya matumizi yasiyo na tahadhari ya
simu pamoja na kompyuta.
Mwanaume anapomwaga
inatakiwa kuwe na seli angalau milioni 20 ili kuweza kurutubisha yai lakini
idadi ya watu wenye kiwango cha chini cha seli hizi inaongezeka kwa kasi.
Shirika la afya la
dunia, WHO linasema ndoa 1 kati ya 5 duniani sawa na 20% wanashida ya kupata mtoto
(ugumba).
Sababu nyingine
zinazoweza kupelekea kuwa na idadi pungufu ya seli za uzazi ni;
- · Uzito mkubwa na kiriba tumbo
- · Matumizi ya madawa ya kulevya
- · Uvutaji wa sigara- Hii huathiri mishipa ya damu
- · Kuendesha baiskeli kwa muda mrefu mara kwa mara
- · Kuendesha vyyombo vya moto kama pikipiki na magari makubwa kwa muda mrefu
- · Kisukari
- · Shinikizo la juu la damu
Dr Nature anashauri,
wanaume kuweka simu zao mbali na korodani. Kama ingelilazimu kukaa nayo
ingewekwa mifuko ya shati/begi. Hii ni kinyume kwa wanawake ambao ni hatari
kuweka simu karibu na maziwa kuepusha kansa ya matiti.
Kama unatamani kuwa
na mtoto panga mapema kwa kuwa na mtindo sahihi wa maisha. “Zaeni Mkaongezeke mkaijaze nchi” ni
kauli ya Mungu aliyetuumba.
Nature Clinic inakutakia uzao mwema!
www.natureclinic.online
[Kama umefurahia
ujumbe huu, tafadhali shirikisha wenzako kadri iwezekanavyo tuokoe wenzetu
wasiofahamu]
No comments:
Post a Comment