• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Wednesday, 4 October 2017

    Kupona Kisukari Inawezekana.. Japo Si Kwa Wote

    Watafiti kutoka Scotland wanasema watu wenye kisukari wanaweza kupona ugonjwa wao kwa kupunguza uzito, lakini wengi wao hawafahamu kama hili linawezakana.

    Kupatikana na aina ya 2 ya kisukari inaweza kuwa ngumu na wengi wanachukulia kwamba haitibiki. Lakini wataalumu wanasema inaweza kutibika kama bado mapema.

    Kama utafuata ushauri wa madaktari na wataalamu wa lishe na ukafanya juhudi kupunguza uzito, kisukari kinaaweza kupona kwa kurudisha kiwango cha damu katika usawa wa kawaida bila dawa yoyote kwa miaka 3-5 ya mwanzo (Dr Sangeeta Kashyap, endokrinolojisti Cleveland Clinic)

    Utafiti ulichapishwa na The BMJ, watafiti wa kiscotland waliarifu kwamba kupunguza uzito wa 15kg (pound 33) inaweza kupunguza na/au kuondoa kabisa kisukari aina ya 2. 

    Watafiti wanasisitiza kwamba uelewa mkubwa, machapisho na ufuatiliaji wa kupunguza ugonjwa huu ingeboresha matokeo ya afya na kupunguza gharama za huduma ya afya.

    Hata hivyo hata kama kisukari kitakwisha kwa kutumia lishe, mazoezi au upasuaji, hali hii haitabaki hivyo milele. Sukari inaweza kuongezeka kufikia ugonjwa wa kisukari tena. Kashyap aligundua hadi 60% ya watu waliopona kisukari kwa upasuaji kisukari kilirudi ndani ya miaka 15.

    Dr Kashyap huwa anawaambia watu kuwa ni likizo bomba ya ugonjwa na tunamatumaini ya kupunguza na kuchelewesha athari za kisukari kama magonjwa ya moyo, macho, figo, na neva.

    Kwa nini kisukari kinarudi?

    Sababu hazifahamiki, lakini inaweza ikawa imesababishwa na kuongezeka uzito au kinasaba. Sehemu ya jibu ni kwamba kongosho hushindwa kuzalisha insulini kadri muda unavyoendelea hii ni kinasaba. Pia, kadri unavyozeeka, kongosho lako huanza kushindwa kufanya kazi. Ndio maana kisukari kinawapata sana wazee.

    Uzito ndio mzizi wa watu kupata kisukari katika umri mdogo. Zaidi ya 82% ya watu wenye kisukari aina 2 wanauzito mkubwa (Dr Kashyap). Sasa kuna vifaa kwaajili ya kupunguza uzito kama lishe, mazoezi, dawa na upasuaji. Huwezi kuzuia usizeeke lakini unaweza kutawala uzito wako.

    Imeandaliwa na Nature Clinic

    No comments:

    Post a Comment