• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Saturday 14 October 2017

    Robo Ya Vifo Duniani Huchangiwa na Hiki


    Shirika la Afya Duniani, WHO linasema watu milioni 12 hufa kila mwaka kutokana na uchafuzi wa hewa, maji, kemikali na mambo mengine ya kimazingira. Karibu robo ya vifo vinavyotokea duniani vinaweza kuhusianishwa na uchafuzi wa mazingira. Shirika la Afya la dunia lilisema katika ripoti yake iliyotolewa Machi 2016.

    Wakala wa afya wanasema inakadiriwa mwaka 2012 watu milioni 12.6 duniani walikufa kutokana na kufanya kazi karibu na maeneo yasiyo salama. Afrika, vifo milioni 2.2 vimehuusianishwa na mambo ya kimazingira kwa mwaka 2016 peke yake. Mambo yanayohusishwa ni uchafuzi wa hewa, maji, na udongo. WHO pia ilionesha kwa upande mwingine moshi, kemikali, mabadiliko ya hali ya hewa, na mionzi ya U.V.

    Maafisa wanasema kuwa mambo yote hayo ya kimazingira huchangia zaidi ya aina 100 za magonjwa na majeraha. Idadi kubwa zaidi ya vifo vinavyohusiana na mazingira hutokea kwenye nchi zenye vipato vya chini na kati Asia ya Kusini-Mashariki, Kusini mwa Pasifiki, na Afrika.

    WHO iliripoti asilimia kubwa ya vifo vinavyotokana na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu na saratani. Hivi vili[patikana zaidi katika nchi zenye kipato cha juu Ulaya, America ya Kusini, na America ya Kasikazini.

    "Mazingira yenye afya hutupatia watu wenye afya" Dr. Margaret Chan, mkurugenzi mkuu wa WHO alisema. "Kama nchi hazitachukua hatua kuweka mazingira wanamoishi na kufanya kazi salama, mamilioni wataendelea kuwa wagonjwa naa kufa angali wadogo".

    Watoto wadogo na wazee wapo katika hatari zaidi ya kufa kutokana na athari za mazingira. Maambukizi ya mfumo wa upumuaji wa chini, magonjwa yanayohusiana na kuhara huwapata sana watoto. Wazee hupata magonjwa yasiyoambukiza kama kiharusi, magonjwa ya moyo, saratani, na magonjwa sugu ya mfumo wa upumuaji.

    Watafiti wanasema inakadiriwa vifo milioni 1.7 vya watoto chini ya miaka, na milioni 4.9 ya watu wazima miaka 50-75, vingekingwa visitokee kwa kutunza vema mazingira. Inakadiriwa kuwa vifo milioni 8.2 vinahusianishwa na uhafifu wa ubora wa hewa. Hii inahusisha na kuvuta hewa iliyoathiriwa na moshi wa tumbaku.

    Njia nafuu za kupunguza matatizo haya ni kujali usalama wa maji, usafi wa vyoo na maji taka, kuongeza chanjo, na matumizi ya vyandarua vilivyotibiwa, kulingana na maelezo ya maafisa wa WHO. Njia nyingine ni kupunguza matumizi ya fueli yabisi kwa ajili ya kupikia na kuongeza upatikanaji wa teknolojia ya nishati kwa kaboni-kidogo.

    Kuna uhitaji wa haraka sana kuwekeza katika mbinu za kupunguza hatari za kimazingira katika miji yetu, nyumbani na sehemu za kazi" Dr. Maria Neira, mkurugenzi wa idara ya afya ya jamii, mazingira na viashiria vya kijamii vya afya, WHO alisema.. "Uwekezaji huo unaweza ukapunguza sana wimbi kubwa linalokuua la magonjwa ya moyo na mishipa ya damu na mfumo wa upumuaji, majeraha, na saratani, na kusaidia kupunguza bajeti kubwa ya huduma za afya.

    Kuongeza upatikanaji wa maji salama, kuongeza juhudi katika usafi, na kuhamasisha uoshaji wa mikono pia itasaidia, walisemaa maafisa wa WHO.

    Tutunze mazingira ili pia yatutunze! Viongozi wa nchi na serikali, wadau binafsi na wale wa umma na mtu mmoja mmoja tunasehemu ya kufanya ili Tanzania iwe nchi salama ya kuishi. Fanya sehemu yako kwa moyo na Mungu atakubariki sana.

    Nature Clinic Tunakutakia Kuwajibika Kwema kwa ajili ya afya zetu..

    WASHIRIKISHE WENGINE KATIKA MITANDAO YA KIJAMII ILI KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUTUNZA MAZINGIRA YETU.

    No comments:

    Post a Comment