• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Monday, 16 October 2017

    TIBA NYUMBANI- Vipele na Miwasho Baada ya Kunyoa

    Watu wengi hupata shida sana baada ya kunyoa. Shida hii inaweza ikawa katika namna mbalimbali na hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine. Mara nyingi shida hii inakuwa folliculitis (yaani maambukizi katika mizizi ya nywele) na huweza kuathiri rika zote. Japo inaweza kuwa inawasha sana na haionekani au haionekani, folliculitis inaweza kutibika nyumbani.

    Visababishi

    Msuguano wakati unanyoa unaweza kuumiza mizizi ya nywele (hair follicles), ambayo inaweza ikavamiwa na bakteria au fangasi kama vile staphylococcus. Folliculitis inaweza pia ikatokea wakati nywele zinapokua na kujikunja nyuma kwenye ngozi. Hata kama hujanyoa hivi karibuni, inaweza ikatokea kutokana na msuguano wa nguo kwenye ngozi au kutoka jasho sana.

    Tiba

    Mara kadhaa kwa watu wengi follicilitis hupotea yenyewe baada ya muda fulani; hata hivyo kama vipele vinakunyima raha au havionekani, itakupasa kuwahisha uponyaji wake. Kanda kwa maji ya moto sehemu husika mara kadhaa kwa siku na osha kwa sabani yenye antibakteria. Unaweza pia ukatumia Hyrocortisone cream au oatmemal-based lotion kuondoa miwasho.

    Kinga

    Kama unanyoa mara kwa mara, folliculitis inaweza ikawa vita yako kila siku. Ili kujikinga na hatari hii, tumia wembe mkali, na msafi kila unyoapo au jaribu kutumia wembe wa umeme. Eneo lililonyolewa litunze katika hali ya usafi kadri iwezekanavyo kwa kuosha mara kwa mara au kufuta kwa kutumia antibakteria toner, na epuka kutumia maji yaliyohifadhiwa kwenye tanki kwa muda mrefu kuoshea kwa sababu yanaweza kuwa yametunza vimelea hawa kwa wingi.


    Onyo!

    Pamoja na kwamba folliculitis huisha yenyewe, wakati mwingine inaweza isipone kwa matibabu ya kawaida ba kusambaa sehemu zingine za mwili. Mtaarifu daktari au mtaalam wa afya kama itaendelea kwa siku 2-3 za kujitibu mwenyewe au kama unajisikia homa au kujisikia joto au maumivu kwenye eneo lililoathirikaa.

    Bofya kitufe cha SHARE na wengine pia!

    No comments:

    Post a Comment