Chanjo ya inayoweza kuzuia saratani. Hadi sasa, chanjo pekee iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kuzuia saratani ni ile ya HPV. Hata hivyo, huzuia dhidi ya virusi vya papiloma ambavyo hupelekea saratani ya shingo ya kizazi, na sio saratani yenyewe.
Lakini utafiti mpya unaofanyika Marekani, ukihusisha hosptali ya Mount Sinai ya New York, unachunguza kugundua chanjo inayoweza kutumia mfumo wa kinga kupambana na seli za saratani zisiwe uvimbe. Mjaribio haya yapo hatua ya 2. Katika hatua hii, wataafiti wanaangalia dalili za ufanisi wa chanjo hii.
Dawa zingine zinazoitwa "checkpoint inhibitors"- ambazo zimeleta mapinduzi katika mfumo wa kinga- zimethibitishwa kutibu baadhi ya saratani, kama vile ya mapafu. Na sasa majaribio ya chanjo, tunatarajia kuleta mavumbuzi katika mfumokinga kupambana na saratani kwa kutumia chanjo itaokoa maisha.
Utafiti huu unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Wewe unamaoni gani kuhusu haya makala? Kama una swali pia unaweza ukauliza.
No comments:
Post a Comment