• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Monday, 23 October 2017

    Je, Chakula Cha siku za Usoni Kitatengenezwa kwa Vidudu na Umeme?


    Watafiti wametengeneza protini ambayo ina viambata vingine vichache sana. Ambayo ingeweza kutumika wakati hali ya hewa itakapoanza kuathiri mazao yetu.

    Athari za mazingira hivi karibuni zitaanza kuathiri sehemu kubwa ya maisha yetu ya kila siku, zaidi chakula. Kama matokeo, chakula cha siku za usoni kitaonekana tofauti sana na kiwango cha virutubisho kuanza kushuka.

    Kutafuta suluhisho, watafiti wa Finland wameweza kutengeneza chakula chenye aina ya nishati kutoka kwenye hewa nyembamba tu. 

    Watafiti kutoka chuo cha teknolojia Lappeenranta na chuo cha ufundi Finland (VTT), walitumia vidudu (microbes), umeme, maji na carbon dioxide kuongeza protini katika vifungashio vya kikombe  cha kahawa.

    Hapa Tanzania kuna kundi la vijana ambao pia wanafanyia kazi mradi wa kutengenza protini kutokana na vidudu/vimelea fulani.

    Lengo la bidhaa  hizi si kuongeza radha bali kutengeneza protini ambayo haihitaji sana hali ya mazingira au kutumia nishati kubwa kuzalisha. Ili kufanya hivyo wanataka kuifanya iwe na ufanisi zaidi kuliko hata ile ya mimea. Watafiti wanafikiria kutumia michakato ya kiumeme ambayo itaongeza ufanisi zaidi ya mara 10 ya ule wa kawaida wa fotosinthesisi.

    Kwa hiyo, haitahitaji sana mazingira kuliko mfumo uliopo wa wanyama, ambao hutumia eneo kubwa sana kwa ajili ya kutunza na kulisha mifugo.

    Kulingana na mila na tamaduni zetu hasa za kitanzania kula baktaria, fangasi au protozoa ni changamoto. Lakini mbona tunakula uyoga wenye protini kwa wingi lakini pia ni fangasi. Hamila nayo ni fangasi, huenda teknolojia hii itakuwa na msaada mkubwa sana siku za usoni.

    Wewe unasemaje? (Tuandikie maoni yako sehemu ya comment hapa   chini)

    No comments:

    Post a Comment