Unataka kuishi angalau miaka mingi kidogo?
Au kubaki na akili safi unapofikia miaka 70, 80 au hata 90?
Huenda unatakiwa kuchora picha na kuzipaka rangi.
Au pengine ungejifunza kupiga kinanda/piano. Kuwa mbunifu inaweza kuifanya miaka yako ya uzeeni kuwa yenye furaha.
Ubongo wa binadamu umebuniwa kukua na kubadilika katika kipindi chote cha maisha ya mtu. Lakini, ubunifu wako unaweza kuboresha hali hii kadri unavyozeeka. Inaweza pia ikakusaidia kuondoa magonjwa mengi ikiwemo yale ya akili. Hata hivyo kuna kweli za kisayansi zinazokubaliana na hali hii.
Tafiti Juu ya Ubunifu na Kuuzeeka
Mwaka 2006, Kituo cha uzee, Afya na Ubinadamu cha Marekani kilitoa taarifa yake iliyoitwa "Utafiti juu ya ubunifu na kuzeeka".
Utafiti huu ulilenga kuainisha matokeo ya ushiriki katika shughuli za kitamaduni. shughuli za kisanaa kwenye afya kwa ujumla, afya ya akili, na maisha ya kijamii ya wazee. Shughuli zilihusisha uchoraji, kucheza, maigizo, mashairi, na muziki.
Hitimisho katika utafiti huo ulionesha kwamba, kuongezeka kwa shughuki za kijumuia/kijamii, zilikuwa na athari chanya katika kuongezaa uhuru na kupunguza utegemezi wa wazee.
Nguvu ya Misuli Yako ya Akili
Kadri unavyoufanyisha mazoezi ubongo wako, ndivyo mitandao mipya inavyoanzishwa, na uwezo wa kufanya kazi huongezeka. Kwa hiyo kujihusisha katika shughuli za kiubunifu itakusaidia katika kuufanyisha mazoezi ubongo.
Kwa ufanisi mkubwa zaidi na kizazi bora kijacho, mambo haya ya sanaa yasisitizwe kwa watoto. Waepushe watoto wako na michezo ya video ya kopyuta na simu na waelekeze kusoma vitabu, sanaa ya muziki, uchoraji na zingine kadri ilivyorahisi kwako.
Wewe unasemaje kuhusu hili? Tuandikie hapa maoni yako.
No comments:
Post a Comment