• Breaking News

    USHAURI, ELIMU na TIBA YA ASILI +255 767-759-137

    Tuesday, 23 May 2017

    Fangasi sehemu za siri (vaginal thrush)



    Ugonjwa huu husababishwa na wadudu wanaoitwa candida na kawaida kila mwanamke anakuwa na jamii ya fangasi sehemu zake za siri na wadudu hao huwa wanamlinda mwanamke ili asishambuliwe na wadudu wengine.

    Inapotokea wale wadudu wanaomlinda kuwa wengi sana ukeni badala ya kulinda mwili hugeuka na kuanza kushambulia na mwisho dalili hujitokeza na ndipo hapo tiba huwa inahitajika haraka sana ili kuzuia madhara mengine.

    Kuna baadhi ya sababu zinazo sababisha fangasi kutokea ukeni na sababu hizo ni kama ifuatavyo:

    Kutumia dawa za antibayotiki mara kwa mara na kwa muda mrefu, husababisha fangasi kwani dawa hizo huua wadudu wote wanaolinda mwili na kuacha uke ukiwa hauna kinga. Dawa za antibayotiki ni kama, Ampicillini, Amoxylline, Ciproflaxine, Doxylline, Erythromycine, Gentamcycine na nyingine nyingi hivyo basi, jamii isitumie ovyo dawa za antibayotiki bila ushauri wa daktari.

    Sababu nyingine ni unene kupita kiasi. Mtu akinenepa anaweza kupata fangasi kwasababu unene husababisha jasho sehemu za siri nakuongeza unyevunyevu sehemu hizo pia michubuko kutokana na kubanwa na nguo ya ndani. Sababu zingine ni utumiaji wa dawa ya jamii ya steroid, dawa hizi ni kama Prednisoline, Hydrocortisone Dexameltasone na nyingine nyingi.
    Hizi nazo hupunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi kuzaliana kwa wingi.

    Pia kuna magonjwa yanayosababisha kupungua kwa kinga nayo ni kisukari, Ukimwi na magonjwa mengine yanayopunguza kinga ya mwili na kusababisha magonjwa nyemelezi.

    Kuwepo na joto kupita kiasi na kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka pia husababisha fangasi sehemu za siri.

    Sababu ni nyingi na hatuwezi kuzitaja zote.


     Dalili zake

    Dalili hutofautiana kutokana na mtu na mwingine ila dalili kubwa ni kutokwa na majimaji meupe wakati mwingine kama mgando wenye rangi ya njano ukiwa umeambatana na muwasho sehemu za ndani au kwenye mashavu ya sehemu za nje za siri.

    Nje ya sehemu hizi za siri hutokea wekundu na maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa.

    Pia mgonjwa atajikuta akikojoa mara kwa mara. Tiba na ushauri Fangasi hutibika vizuri nakupona ila ni vizuri ukaenda hospitali na kufanyiwa kipimo cha mkojo ambapo chembechembe za yeast huonwa vizuri kwenye darubini.

    Usitumie dawa bila maelekezo ya daktari unaweza kusababisha hali kuwa mbaya zaidi  au kuongeza matatizo ambayo haya kuwepo kabla.

    Wako,
    Dr Nature

    No comments:

    Post a Comment