kifafa cha mimba
Kifafa cha mimba (eclampsia) inachangia 1/3 ya vifo vya watoto kabla ya kujifungua na wale wanaokufa muda mfupi baada ya kujifungua katika ulimwengu wa 3 ikiwemo Tanzania. Tatizo hili huanza kwa kuongezeka kwa shinikizo la damu kwa mama hali ambayo inaitwa pre-eclampsia. Mara nyingi msukumo huu wa damu unaweza kuwa kuanzia 140/90mmHg japo kwa baadhi ya watu huwa hadi 150/90 mmHg.
Mgandamizo ukiendelea kuwa mkubwa zaidi unaweza kusababisha kuachia kwa kondo la nyuma (placenta) na hivyo kifo cha mtoto.
Pre-eclampsia (kuongezeka kwa shinikizo la damu kupita kiasi) hutokea kuanzia wiki 20 ya ujauzito na hasa wiki 24 kwa wengi.
Unataka kupunguza uzito na kitambi bila kufanya mazoezi? BONYEZA HAPA
Chanzo cha kifafa cha mimba.
Sababu zinazosababisha kifafa cha mimba mpaka sasa haziko wazi, japo mambo yafuatayo yanaweza kupelekea mtu kupata kifafa cha mimba:
- Matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjammzito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba.
- Imegundulika kuwa ikiwa mwanamke atazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka. Hii ni kwasababu ya michakato ya kinga za mwili.
- Mimba ya kwanza ya mama imeonekana kuhusianishwa na msukumo mkubwa wa damu na wakati mwingine kifafa.
- Historia ya mtu kuwa na kifafa cha mimba katika familia/ ukoo wenu.
- Kama unaumri chini ya miaka 20 au zaidi ya miaka 40 wakati wa ujauzito.
- Kama ulikuwa na tatizo la shinikizo kubwa la damu kabla ya ujauzito.
- Kama una uzito mkubwa (BMI) au kiriba tumbo.
- Kama unahistoria ya kifafa cha mimba wakati uliotangulia.
- Mimba ya mapacha.
Dalili za kifafa cha mimba.
Ukiona dalili hizi mwone mtaalamu kwa uchunguzi.
- Maumivu makali ya kichwa.
- Kuvimba miguu.
- Maumivu ya chembe moyo (epigastric pain).
- Kushindwa kuona vizuri (blurred vision).
- Mapigo ya moyo wa mtoto kushuka.
- Kutokukua vizuri tumboni (intrauterine growth restriction)
- Maumivu ya tumbo juu ya kitovu.
- Kutapika
- Mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida.
- Kupumua kwa shida.
- Uchovu na maumivu ya viuno.
- Kupoteza fahamu na degedege.
Matokeo ya kifafa cha mimba.
- Mtoto kufia tumboni.
- Figo kufeli.
- Seli chembe sahani za mama kupungua hivyo damu kushindwa kuganda anapopata jeraha. Hii inaweza sababisha mama kupoteza damu nyingi na hata kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
- degedege/kifafa kwa mama.
- Kuchanganyikiwa na kupoteza fahamu.
Tiba ya kifafa cha mimba.
Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa placenta ndani ya kifuko cha kizazi ambayo haiko sawa. Bila kuondoa placenta mgonjwa hatapona.
Ikiwa mtoto bado hajawa tayari kwa kuzaliwa, daktari anaweza kumshauri mama alazwe ili kupata uangalizi wa karibu mpaka mtoto atakapo komaa. Pia daktari anaweza kumshauri mama apewe dawa za kuharakisha kukomaa kwa mapafu ya mtoto.
Iwapo hali ya mjamzito itakuwa mbaya zaidi, daktari anaweza kumzalisha hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari ya mtoto kufia tumboni, mama kupata degedege na kupoteza fahamu, pia kupoteza damu nyingi kwa sababu damu hupoteza uwezo wa kuganda, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, mjamzito kupata kiharusi (stroke) na kupoteza maisha.
Ushauri.
Mama unapaswa kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kupimwa na maendeleo yako na mtoto yfahamike na ikiwa kama kunashida yoyote upate msaada wakitabibu mapema.
Mwanamke kuwa mwaminifu kwa mume wako! Sio tu kwamba itakusaida kupunguza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba lakini pia matatizo mengi ya kijamii na kiafya.
Kwa ushauri wa kiafya BURE wasiliana nami Dr Nature
simu: +255 767 759 137
yusuphmfilemon@gmail.com
All rights reserved
2017
No comments:
Post a Comment