Nimetamani sana kuwaletea somo hili enyi rafiki zangu kutokana na maneno mengi ninayosikia kuhusu soya.
Kusema kwamba soya ni salama au la inategemea unamsikiliza nani. Ukisoma kwenye intaneti kuna website nyingi zinazoelezea na kuna pande 2 zinavutana, kati ya wazalishaji wa soya na wazalishaji wa mazao ya maziwa.
Soya inafaida nyingi sana za kiafya kutokana na wingi wa protein na madini yaliyomo ndani yake.
Tafiti za kiepidemiolojia zinaonesha kuwa matumizi ya soya hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya saratani.
Pia matokeo yalionesha kuwa soya husaidia kupunguza kiwango cha lehemu (cholesterol) kwenye damu kwa hiyo husaidia kuepusha magonjwa ya moyo na mishipa ya damu .
Tafiti zinaonesha pia soya husaidia kulinda mwili dhidi ya saratani zanazohusiana na vichochozi (homoni) na magonjwa yake kama maumivu wakati wa hedhi na miwasho wakati hedhi inapokoma.
Zaidi, mamilioni ya watoto wamekuwa wakipewa lishe ya soya toka miaka ya 1930 bila ushahidi wa madhara yoyote.
Upande wa pili>>>
Haya ni ya kuogopesha yabayosemwa kuhusu soya :
Homoni ya mmea estrogen iliyopo ndani ya soya unaweza kumfanya mtoto wa kiume akawa na tabia za kike; na kwamba huongeza uwezekano wa kupata saratani ya matiti, soya huongeza uwezekano wa kupata shida kubwa ya tezi ya thairoidi ikiwemo saratani na mengine.
SASA NANI YUPO SAHIHI?
Hakuna matokeo dhahili ya kiutafiti ya kiepidemiolijia kuunga mkono athari za matumizi ya kawaida ya soya.
Hata hivyo pamoja na faida tajwa, kiasi katika matumizi ya soya kizingatiwe. Kikombe kimoja cha maziwa ya soya kwa siku kinatosha kabisa maana #too much is harmful#
Pole kama nimekuchanganya na sasa unakosa kipi ndio cha kufanya....
Kanuni rahisi ni hii:
Fanya milo yako iwe rahisi, na ya kubadili badili aina ya vyakula, ukipendelea sana wanga isiyokobolewa, matunda na mboga mboga nyingi na kiwango kidogo cha maharage na jamii zake, karanga na jamii zake, mbegu mbegu itakusaidia sana kuepuka matatizo mengi yanayotokana na lishe, ikiwemo ya soya.
Wakati mwingine tutajifunza namna sahihi ya kuandaa soya kwa chakula.
#Fanya kila uwezalo kula ukiwa na moyo wa shukrani | Do the best that you can and eat with a thankful heart
•••••••••••••••••••••••••
Pata masomo mengine zaidi kuhusu AFYA YAKO hapa>>>>naturefreeclinic.blogspot.com
Nature Treats Love Heals
No comments:
Post a Comment