Hebu jiulize kidogo, toka umezaliwa siku imewahi kupita bila kula wala kunywa?
Duuh! wewe ni hatari! Na umri wote huo kila siku unakula tu? Hata mwili wako unahitaji kupumzika.. Haya hebu tuone kufunga inakuwaje na faida kiafya.
Kwa kawaida kufunga limekuwa ni kitendo ambacho kinasauti kubwa ya dini. Watu katika dini zao hufunga ili kuonesha nia zao njema mbele za Mungu. Lakini kuna wengine ambao hufunga ili kupunguza uzito/mwili. Wote hawa wapo sahihi lakini Mimi nitakazia zaidi kuonesha faida za kufunga.
FAIDA ZA KUFUNGA KIAFYA✍
Kufunga hupumzisha na/au kuondoa siku katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ini.
Husaidia mtu kujijengea uwezo wa kujitawala katika kula (kuwa na kiasi), kitu ambacho ni kizuri sana kama unaparangana kupunguza uzito au shida zingine za kiafya.
Funga fupi inaweza ikawa msaada sana kwa mtu mwenye MSONGO, ALIYECHOKA AU KUJISIKIA VIBAYA BILA SABABU MAALUMU.
Kuna namna nyingi za kufunga jichagukie moja unayotaka na uanze kufanya:
a) kukosa mlo mmoja
b) kukosa Milo ya siku nzima huku ukinywa maji na chai tu
c) kukosa Milo ya siku nzima bila kuingiza chochote kinywani
d) kutumia matunda tu kwa siku 2- 7. Hii ni funga ambayo naipendekeza kwako maana Mimi nilipofanya nilipata mrejesho kutoka kwa rafiki zangu kuwa nikilikuwa ninang'aa na kuonekana mtoto/kijana zaidi. Hii ni dalili kwamba mwili umesafishwa na ini lipo safi ndio maana hata ngozi inang'aa.
Ushauri wangu kwa wale wanaotumia vipodozi sana ili wang'ae nadhani wanatumia nguvu nyingi na gharama kubwa kuharibu ngozi zao kwa kutumia vipodozi vikali, pole sana! Fanya hivi halaf utanipatia majibu ndani ya siku 7. Funga kwa kutumia njia hii utashangaa maajabu yake.
Hii pia itakusaida sana kuweza kuepuka magonjwa mengi yaliyokuwa yanakunyemelea na utakuwa umeongeza kinga ya mwili.
Wale wenye uzito mdogo kupita kiasi wawe makini na mifungo lakini wenye uzito mkubwa wanaofanya bidii kupunguza funga za Mara kwa Mara zitawasaidia sana.
# Nafaka, matunda, Karanga na jamii zake na mbogamboga vina virutubisho vilivyochaguliwa na MUUMBA wetu. Vyakula hivi, vilivyoandaliwa katika namna rahisi na asili kwa namna iwezekanayo, ni vyakula bora na vyenye afya kuliko vingine vyote.
Karibu tena naturefreeclinic.blogspot.com
Nature Treats Love Heals
No comments:
Post a Comment