Ili mtoto wako awe na afya njema wakati wa utotoni na Siku za usoni haya ni muhimu..
1. Anapozaliwa tu, anatakiwa apewe maziwa ya mwanzo (colostrum) wengine huyaita maziwa mchafu. Kwa hiyo mama hayo maziwa usiyamwage tafadhali ni zawadi kwa mtoto wako.
Faida zake
- Hupakaza rangi kwenye kuta za mfumo wa chakula ili usiharibiwe na chakula kitakachokuja baadaye
- kuongeza kinga ya mwili ya mtoto wako.
- ni chakula kizuri chenye virutubisho vyote muhimu kwa mtoto.
2. Baada ya hapo mtoto anyonyeshwe bila kupewa maji wala chakula chochochote kwa miezi 6.
3. Baadaye mtoto aendelee kunyonyeshwa kwa muda zaidi huku akipatiwa chakula laini kwa namna nyingi mchanganyiko.
Vyakula vinavyomfaa mtoto
Ni chakula chenye calories nyingi (nguvu) sana, nyuzinyuzi kidogo. Vyakula vya wanga vyenye nyuzinyuzi kidogo ni wali na ndizi... Hivi kila mtoto asinyimwe!
Pia karanga au jamii zake zilizosagwa vizuri, na mbegumbegu kV maboga, alzeti zinaweza kusagwa na kuongezwa kwenye maziwa ili kuongeza calories..
Watoto wanahitaji calories nyingi kwa sababu miili yao bado inakuwa na hivyo inashughuki nyingi sana zenye kuhitaji nguvu nyingi.
Uji wa soya na mchanganyiko wake (unga lishe) .. Waoh usimnyime mtoto!
*Faida za kumoatia mtoto wako vyakula vingi vya mimea na sio wanyama*
Zina virutubisho vingi ikiwemo madini ya chuma, vitamin C, ambayo inasaidia ufyonzwaji wa madini ya chuka, na kemikali zingine muhimu sana (phytochemical) zilizopo kwenye mimea, ambazo huimarisha kinga ya mwili ya mtoto dhidi ya maradhi. Ataeouka kiriba tumbo na magonjwa yake kV moyo, kiharusi, kisukari, saratani n.k
Unataka mtoto wako awe na afya njema ya akili na mwili hadi Siku za usoni?
Mpatie vyakula vinavyotokana na mimea. Lakini kuwa makini katika uchaguzi wake. Ukiamua kutumia mazao ya kimea tu kama chakula lazima upate supplement ya vitamin B12 ambayo haipatikani kwenye mimea na ni muhimu sana.
ONYO:
Usimpatie mtoto chochote kingine zaidi ya maziwa ya mama wa binadamu ndani ya miezi 6.
Akishafikisha miezi 6, chakula cha mtoto kiwe rahisi na kuwa mwangalifu usimjaze na mlo wenye vyakula vingi vyenye nguvu kidogo, nyuzinyuzi nyingi na mbogamboga.
# KUMBUKA ZAWADI YA KWANZA YA MTOTO SIKU ANAPOZALIWA NI CHANJO!
No comments:
Post a Comment