Vyakula vyenye afya kuliko vyote duñiani ni vilivyojikita zaidi kwenye wanga isiyokobolewa, ongeza matunda mengi na mboga mboga nyingi. Bila kuacha nyuma maharage na jamii zake, Karanga na jamii zake na mbegu mbegu. Viandae katika namna rahisi bila kuongeza mafuta yasiyo lazima, sukari au viungo, furahia chakula chako!
*Ni muda gani unatakiwa kula*⏱
Kula kwa ratiba ni muhimu sana kwa sababu mfumo wa chakula hufanya kazi vizuri zaidi kwa ratiba.
Chakula cha kawaida hutumia zaidi ya masaa 4 tumboni. Muda kati ya milo angalau uwe masaa 5 ili kulipatia tumbo muda wa kupumzika na kujipanga kwa kazi nyingine.
Mlo wa usiku uwe mwepesi na uliwe angalau masaa 2 kabla ya kwenda kulala, ili tumbo nalo lipumzike wakati unapolala.
Hii itakuletea usingizi mzito na mtamu na pia kukuongezea hamu ya kula vizuri asubuhi.
*MLO WA ASUBUHI*🕰
Huu ndio mlo mkuu wa siku!
Unatakiwa rahisi, haraka na rahisi kuandaa, lakini wa kutosha. Watu wengi huchagua matunda na mlo wa nafaka - mf. Matunda, nafaka na mbegu mbegu.
NAFAKA:
Kuhusu nafaka chagua iliyoandaliwa bila kukobolewa wala kuongezewa sukari.
MBADALA WA MAZIWA YA WANYAMA
Tumia matunda yaliyopikwa au bila kupikwa, juisi ya matunda, soya na maziwa ya Karanga.
MKATE:
Chagua na badilisha aina ya mikate utakayotumia kila siku ukipendelea Sana iliyotokana na nafaka zisizokobolewa.
VIPAKAZO:
Chagua vile vyenye virutubisho vingi kama vipakazo kwenye mkate wako.
Tumia jibini ya Karanga, parachichi ( ni mbadala bora sana wa jibini ya maziwa na vitu kama blue band), ndizi zilizosagwa, matunda mengine yakipikwa na kusagwa yanafaa sana.
*CHAKULA CHA MCHANA*⏰
Huu pia ni mlo mkuu wa siku. Katika milo yote vitafunwa vidogovidogo kama Karanga, mbegu za maboga, n.k ni hiari (optional).
*Chakula cha mchana cha kupika*
SEHEMU YA WANGA YA KUSHIBISHA
Chagua viazi, wali wa kahawia, pasta, mahindi n.k vilivyopikwa au kuokwa.
MBOGA MBOGA:
Aina mbalimbali na rangi, kula zingine mbichi na zingine zilizolipikwa.
VYAKULA VYENYE PROTINI NYINGI:
Chagua kiasi kidogo cha haya: jamii ya mikunde, jamii ya Karanga, na kundi la mbegu mbegu. Inapendeza ukila pamoja na wali au chakula kingine na pia sio mbaya ukila peke yake katika chombo.
SOSEJI NA UREMBO WA CHAKULA:
Ni muhimu kwa ajili ya kuongeza hamu ya kula, lakini lazima ichaguliwe kwa makini, kwa sababu chache tu ndio salama kiafya kati ya zilizopo dukani.
*Chakula cha mchana chepesi*
WANGA:
Mkate
MBOGA MBOGA:
Supu au/na Salado
PROTINI:
Jibini ya Karanga na jamii zake, au supu ya maharage.
*CHAKULA CHA USIKU*⏰
Ni bora sana kuwa na chakula chepesi sana usiku kama inawezekana. Kwa sababu chakula unachokula usiku huwa kinatunzwa kama mafuta. Chakula kingi cha usiku huliweka tumbo kubanana na shughuli usiku wakati linatakiwa kupumzika.
Unaweza kuchagua matunda na mkate na ukaongeza supu na/au saladi kwenye mkate au ukala matunda tu - yote hii ni mifumo mizuri ya chakula cha usiku.
*Je ule na kunywa?*
Kunywa kinywaji kingi wakati unakuka hasa baridi, hupunguza nguvu ya vimeng'enya na hivyo kupunguza kasi ya kusaga chakula.
Kitu chema ni kunywa kati ya mlo mmoja na mwingine. Kama umekunywa kinywaji kingi kabla ya mlo na wakati wa mlo ukawa na matunda au mboga mboga hutahitaji kinywaji wakati wa kula.
*Vipi kuhusu kuruka mlo?*
Kama huna uzito mdogo kupita kiasi ni jambo jema kuruka mlo maana utalipatia tumbo na mfumo mzima wa chakula pumziko.
Lakini ni kosa kubwa kuruka mlo wa asubuhi mara kwa Mara.
Wakati una msongo, umebanwa na kazi nyingi sana, hujisikii vizuri kwa ujumla, kuruka mlo 1 au 2 ya usiku itakusaidia kuwa vizuri ndio maana wengine huamua kuwa na milo 2 tu kwa siku.
*Je ni sahihi kula mboga mboga na matunda kwa wakati mmoja?*
Watu wengine hupata shida kuvisaga vyote kwa pamoja. Kwa hiyo ni vema ukavitenganisha, kama mlo huu umekula matunda basi mwingine kula mboga mboga. Kwa hiyo jaribu kuchanganya changanya kadri iwezekanavyo.
*Ni kanuni gani ifuatwe katika kuchanganya vyakula?*
KULA VYAKULA VYA AINA MBALIMBALI KADRI UWEZEKANAVYO AMBAVYO NI MAZAO YA MIMEA YASIYOCHAKATWA (KUKOBOLEWA), LAKINI KILA MLO UWE RAHISI NA USILE SANA KUPITA KIASI.
*Sasa nifanyeje kama siwezi kujichagulia menyu ya Chakula nachotaka?*
Kama huna kauli yoyote kuhusu jiko yaani nini kipikwa na nini kiletwe mezani, bado unaweza kufanya uchaguzi ambao utaimarisha mlo na afya yako.
Kwanza, usiongeze sukari kwenye Chakula na epuka vyakula vyenye sukari nyingi. Jipatie vyakula vingine kama matunda na jamii za Karanga badala ya hivyo vya sukari kama inawezekana.
Kuwa makini kuhusu mafuta. Mafuta yanatokana na jibini {butter) unayoweka kwenye mikate, vyakula vilivyokaangwa sana na mafuta. Kumbuka pia ⅓ ya vyakula kama keki, biskuti na icecream ni mafuta na zaidi ni sukari hivi jitahidi kuvikwepa.
Kula sana mboga mboga na saladi na kula kidogo sana vyakula vyenye mafuta mengi.
Usisahau kufanya mazoezi yatakusaidia kuziba mapengo katika afya yako ambayo umeshindwa kuyafikia kwa mlo bora.
*Ni kwa kiasi gani ninatakiwa kuwa na msimamo katika suala la Chakula?*
Hapa ni maamuzi ya mtu binafsi. Kama unataka kutawala uzito, hali ya kijamii na kiuchumi.
Kuondoka mara moja moja katika misingi ya Chakula bora haiepukiki, lakini matumizi ya mara kwa mara ya vyakula visivyofaa huleta ugumu kupata radha ya Chakula kizuri kikiletwa.
Kama ukifanikiwa kuepuka vyakula hatari utajikuta unafurajia radha ya vyakula vya afya.
Kula mara chache kwenye matukio ya kijamii unaweza usiathiwe katika afya yako lakini inapokuwa mara nyingi unajikuta umeanza kuteleza na kunogewa mwisho unaharibikiwa.
# ISIFE MOYO KAMA UNAONA HUWEZI KUFIKIA VIWANGO VYA CHAKULA KAMILI BORA, KWA SABABU YA KUBADILI KAZI, FAMILIA NA MAMBO MENGINE. FANYA KILA LILILO NDANI YA UWEZO WAKO, NA KUMBUKA KUWA MATENGENEZO YA AFYA NI ENDELEVU, NA KUWA TAYARI KUFANYA MABORESHO PALE UTAKAPOWEZA.
Tafadhali nisaidie share kwa wengine wajifunze!
Nature Treats Love Heals
Somo limeeleweka vizur
ReplyDeleteDaah nmependa mafunzo kwanzia wik ijayo najipanga nianze mlo wangu
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu hii nitaifanyia kazi.
ReplyDeleteAhsante sana kwa muongozo huu mzuri. Kitu adimu sana hiki.
ReplyDelete